Senegal kuzindua mpango wa chanjo ya COVID-19 wiki ijayo kwa kutumia chanjo iliyotengenezwa China
2021-02-19 19:08:45| cri

Waziri wa Afya na Jamii nchini Senegal Abdoulaye Diouf Sarr amesema, nchi hiyo itazindua kampeni ya kutoa chanjo ya virusi vya Corona nchini humo Jumanne wiki ijayo.

Akizungumza kupitia televisheni ya umma nchini humo, waziri huyo amesema kampeni hiyo itazinduliwa baada ya kuanzishwa kwa kamati ya usimamizi, na kuwataka Wasenegal kujitokeza kwa wingi kufanikisha kampeni hiyo.

Rais Macky Sall wa Senegal, alipokea awamu ya kwanza ya dozi laki mbili za chanjo ya virusi vya Corona iliyotengenezwa na kampuni ya madawa ya China, Sinopharm.