TENNIS: Naomi amliza Serena Australian Open
2021-02-19 16:58:23| CRI

Mcheza Tennis kutoka Japan Naomi Osaka amemfunga Serena Williams katika mashindano ya nusu fainali ya Australian Open yaliyochezwa jana alhamis. Serena alishuhudia juhudi zake za kutwaa taji la 24 la Grand Slam zikipotea baada ya kufungwa kwa seti 6-3 na 6-4 na Osaka ambaye ni bingwa mara tatu wa taji hilo. Williams amekuwa akiwania kuewka rekodi tangu aliporejea ulingoni baada ya kujifungua mwaka 2018, na tangu wakati huo, ameingia kwenye fainali za Grand Slam mara nne lakini ameshindwa kuchukua ubingwa huo.