Rais wa China akutana na wawakilishi wa chombo cha anga ya juu cha Chang’e -5
2021-02-22 19:30:36| cri

Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing, katika Jumba la Mikutano la Umma, amekutana na wawakilishi wa wanasayansi na wahandisi walioshiriki katika utafiti na uendelezaji wa chombo cha anga ya juu cha Chang’e – 5 kinachotafiti Mwezi.

Rais Xi pia alitembelea maonyesho ya sampuli za Mwezi zilizoletwa duniani na chombo hicho na mafanikio ya utafiti wa China katika Mwezi.