Rais wa Uganda akutana na mwanadiplomasia mwandamizi wa China
2021-02-22 09:23:29| cri

 

 

Rais Yoweri Museveni wa Uganda jana alikutana na mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni mkurugenzi wa Kamati ya mambo ya nje ya Kamati Kuu ya CPC Bw. Yang Jiechi ambaye yuko ziarani nchini Uganda.

Bw. Yang amefikisha salamu za rais Xi Jinping wa China kwa rais Museveni na kumpongeza kwa kushinda tena kwenye uchaguzi wa rais. Bw. Yang pia amesema China iko tayari kushirikiana na Uganda kupambana na COVID-19.

Rais Museveni amesema Uganda inaikaribisha China kuwekeza nchini humo, pia ameeleza matumaini kuwa bidhaa nyingi zaidi za Uganda zinaweza kuingia kwenye soko la China. Vilevile ameshukuru nafasi muhimu ya uzoefu wa China katika kukuza uchumi wa Afrika na kuboresha maisha ya watu barani Afrika.