Watu saba wafariki kwenye mlipuko wa bomu la ardhini kusini magharibi mwa Niger
2021-02-22 08:44:34| CRI

Mlipuko wa bomu la ardhini uliotokea jana Jumapili katika mkoa wa Tillabéri ulioko kusini magharibi mwa Niger, umesababisha vifo vya watu saba.

Shirika la habari la Niger likiwanukuu maofisa wa mkoa huo, limeripoti kuwa mlipuko huo ulitokea baada ya gari la wafanyakazi wa tume ya uchaguzi kukanyaga bomu la ardhini kwenye eneo la Dargol mkoani humo, na kusababisha vifo vya watu saba na wengine watatu kujeruhiwa vibaya. Idara ya usalama ya Niger bado haijatoa tamko lolote kuhusiana na tukio hilo.