China kutoa msaada wa chakula kwa Ethiopia
2021-02-22 19:44:18| CRI

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin leo amesema, China itatoa msaada wa dharura wa mchele na mpunga kwaJimbo la Tigray, Ethiopia ili kupunguza uhaba wa chakula katika mkoa huo.

Bw. Wang Wenbin amesema, China inaunga mkono juhudi za serikali ya Ethiopia za kutoa msaada kwa watu wa jimbo la Tigray na kurejesha uzalishaji na maisha ya kawaida katika jimbo hilo. Pia amesema China inaitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza msaada, na kushirikiana kutoa mchango kwa ajili ya jimbo hilo kurejesha uzalishaji na maisha ya kawaida.