Eneo la Biashara Huria la Afrika latajwa kutoa nyenzo muhimu kwa Nigeria kufufua uchumi
2021-02-22 08:45:05| CRI

Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Kiuchumi nchini Nigeria (NEPZA) imesema Eneo la Biashara Huria la Afrika limetoa nyenzo muhimu kwa Nigeria kuchochea ukuaji wa uchumi.

Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi mtendaji wa mamlaka hiyo Adesoji Adesugba, inasema serikali ya Nigeria itatumia eneo la biashara huria la Afrika kuongeza ushindani wa nchi hiyo kwenye biashara.