Rais wa Algeria afanya mabadiliko baraza la mawaziri
2021-02-22 08:43:53| CRI

Rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria jana Jumapili alifanya mabadiliko baraza la serikali, na kusaini amri ya kuvunja baraza la chini ya bunge.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais, mawaziri saba wamebadilishwa, lakini Bw. Abdelaziz Djerad ataendelea kuwa waziri mkuu. Rais Tebboune amesema uchaguzi wa wabunge utafanyika ndani ya miezi mitatu baada ya kuvunjwa kwa baraza la chini la bunge la sasa.