SOKA: Manchester City waifunga Arsenal na kuanza kunusa taji la EPL
2021-02-22 15:48:36| cri

Kocha Pep Guardiola amesema anashangazwa na ubora wa fomu ya kikosi chake cha Manchester City wakati wapinzani wao wakuu katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) wakisuasua. Chini ya Guardiola, Man-City haijapoteza alama yoyote tangu Disemba 15, 2020 na ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Arsenal katika mechi iliyochezwa jana kwenye uwanja wa Emirates uliwasaidia kuweka pengo la alama 10 kileleni mwa jedwali. Zikiwa zimebaki mechi 13 pekee kwa ligi ya EPL muhula huu kumalizika rasmi, Man-City kwa sasa wanajivunia alama 59, wakifuatiwa na Manchester United kwa pointi 49 sawa na Leicester City.