SOKA: Rashford, Fernandes wacheka na nyavu huku Man United ikiifunga Newcastle 3-1
2021-02-22 15:48:15| cri

Manchester United mnamo Jumapili, Februari 21 usiku, walisajili ushindi wa 3-1 dhidi ya Newcastle United na kurejea nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu. Newcastle walikuwa wanapigana kumaliza wenyeji wa Old Trafford lakini Mashetani Wekundu ndio walizoa alama zote tatu kutokana na magoli ya Marcus Rashford, Daniel James na Bruno Fernandes. Ushindi huo uliwashuhudia wakirejea kwenye nafasi ya pili jedwalini na alama 49 lakini bado mahasidi wao Manchester City, wameweka pengo la alama 10 kileleni.