Rais wa Tanzania awataka wananchi wavae barakoa
2021-02-22 09:05:09| CRI

Rais John Magufuli wa Tanzania jana aliwataka wananchi waendelee kuchukua hatua za kujikinga dhidi ya maambukizi ya COVID-19 kama inavyoagizwa na wataalam wa afya, ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa.

Akiongea mjini Dodoma kwenye misa ya jumapili, Rais Magufuli alisema serikali haijazuia watu kuvaa barakoa kama moja ya njia ya kujikinga dhidi ya virusi vya Corona. Taarifa iliyotolewa na kurugenzi ya mawasiliano ya Rais ya ikulu ya Tanzania, imesema rais Magufuli amependekeza wananchi kutumia barakoa zilizotengenezwa Tanzania.

Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsi, wazee na watoto ya Tanzania pia imewataka watu waendelee kuchukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kunawa mikono na kutumia vitakasa mikono.