Niger yafanya duru ya pili ya uchaguzi wa rais
2021-02-22 11:24:32| CRI

Niger jana ilifanya duru ya pili ya uchaguzi wa rais, ambapo mgombea wa chama cha demokrasia na ujamaa cha Niger Bw. Mohamed Bazoum na rais wa zamani wa nchi hiyo Bw. Mohamane Ousmane waliopata kura nyingi katika duru ya kwanza wanagombea nafasi hiyo katika duru ya pili.

Vituo 26,000 vya kupigia kura kote nchini Niger vilifunguliwa tarehe 21 saa 2 kwa saa za huko na kufungwa saa 1 jioni, na idadi ya raia waliojiandikisha kupiga kura ilizidi milioni 7.4. Niger iliimarisha hatua za usalama kwenye vituo hivyo ili kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika bila matatizo.

Rais wa sasa Mahamadou Issoufou alitoa taarifa akisema Niger itatimiza mabadiliko ya uongozi kwa utulivu na kutaka uchaguzi huo ufanyike kwa haki na uwazi.