China kutoa chanjo ya COVID-19 kwa nchi 19 za Afrika
2021-02-22 18:38:03| cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema, China itatoa chanjo ya virusi vya Corona kwa nchi 19 zaidi za Afrika, na kwamba ushirikiano wa kimataifa wa China katika chanjo unalenga kuifanya chanjo hiyo kuwa bidhaa ya umma.

Wang amesema hayo alipotakiwa kuzungumzia madai ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika Mkutano wa Usalama wa Munich kuwa Ulaya na Marekani zinapaswa kutoa chanjo za kutosha za virusi vya Corona kwa Afrika, bila ya hivyo nchi za Afrika zinaweza kuchagua kununua chanjo kutoka China na Russia, akisema kuwa nguvu ya Magharibi itakuwa ya kufikirika, na sio uhalisia.