SOKA: Monaco yaichapa PSG 2-0 kwenye Ligue 1
2021-02-22 15:48:55| cri

Kikosi cha AS Monaco kiliwaduwaza Paris Saint-Germain (PSG) kwa kuwapa kichapo cha bao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) iliyochezwa jana usiku katika uwanja wa Parc des Princes. Mechi hiyo ilikuwa ya pili kwa kocha Mauricio Pochettino kupoteza akiwa kocha wa PSG tangu aaminiwe kuwa mrithi wa Thomas Tuchel aliyekwenda Chelsea baada ya kupigwa kalamu mnamo Disemba 24, 2020. Sofiane Diop aliwafungulia Monaco ukurasa wa mabao katika dakika ya sita alipokamilisha krosi ya Ruben Aguilar aliyeshirikiana vilivyo na fowadi Kevin Volland. Guillermo Maripan alizamisha kabisa matumaini ya PSG kurejea mchezoni kwa kufunga bao la pili la Monaco katika dakika ya 51 baada ya kuchuma nafuu kutokana na masihara ya kiungo Ander Herrera aliyeshindwa kuondoa mpira katika eneo la hatari.