SOKA: Mechi kati ya timu ya Algeria na Afrika Kusini kuchezwa Uwanja wa Mkapa
2021-02-22 15:47:05| cri

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema mechi kati ya CR Belouizdad kutoka Algeria dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini itachezwa katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, Tanzania. Mechi hiyo ni hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na itachezwa jumapili ya tarehe 28 mwezi huu. TFF imesema uamuzi huo umekuja baada ya Belouizdad kutuma maombi ya kutaka kutumia Uwanja wa Mkapa kama uwanja wake wa nyumbani kwa mechi hiyo, ombi ambalo limekubaliwa na TFF baada ya kushauriana na serikali.