Mjumbe wa China apinga kauli za kupotosha za ofisa wa Uingereza katika kikao cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa
2021-02-23 17:15:23| cri

Ujumbe wa China katika Ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva umepinga kauli za kupotosha kuhusiana na China zilizotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza katika mkutano wa 46 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ulioanza jana.

Msemaji wa Ujumbe huo, Liu Yuyin amesema kuwa, haki za binadamu hazipaswi kutumika kwa ajili ya malengo ya kisiasa, na wala sio chombo cha kuchafua nchi nyingine na kuzuia maendeleo yao. Amesema maofisa kutoka Uingereza, Ujerumani, Denmark na Finland na baadhi ya nchi nyingine chache wametumia vibaya jukwaa la taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa kwa kueneza taarifa za uongo, kuichafua China na kuingilia mambo ya ndani ya China, na China inapinga kimsingi kauli zao.

Liu amesema, Xinjiang na Tibet ni mikoa ambayo watu wa makabila madogo wanaishi, na ni mfano mzuri wa maendeleo ya haki za binadamu nchini China, na kuongeza kuwa China inatafuta sera ya kikabila inayozingatia usawa, umoja, kujiendesha kwa mikoa ya makabila hayo, na ustawi wa pamoja.