Rais wa Zambia akutana na mwanadiplomasia mwandamizi wa China
2021-02-23 09:31:27| CRI

Rais Edgar Lungu wa Zambia jana alikutana na kufanya mazungumzo na mjumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China CPC na mkurugenzi wa ofisi ya kamisheni ya mambo ya nje ya kamati kuu ya CPC Bw. Yang Jiechi ambaye yuko ziarani nchini humo.

Bw. Yang alifikisha salamu za rais Xi Jinping kwa rais Lungu, na kusema tangu kutokea kwa janga la COVID-19, China na Zambia zimekuwa zikisaidiana na kushinda matatizo kwa pamoja, na kuonyesha maana halisi ya marafiki wazuri, washirika wazuri, na ndugu wazuri kwa hatua halisi.

Rais Lungu amesema Zambia inaishukuru China kwa kuipatia msaada na uungaji mkono wa muda mrefu, itaendelea kuunga mkono sera ya kuwepo kwa China moja na inapenda kuimarisha ushirikiano na China, ili kuwanufaisha watu wa nchi hizo mbili.