Marais wa China na Misri wafanya mazungumza kwa njia ya simu
2021-02-23 09:10:05| CRI

 

 

Rais Xi Jinping wa China jana usiku alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Misri Abdel-Fattah al-Sisi.

Kwenye mazungumzo yao rais Xi amekumbusha historia ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na kusema China inapenda kuimarisha uratibu na Misri katika mambo ya kimataifa na kikanda, na kulinda kwa pamoja utaratibu wa pande nyingi na haki za kimataifa. Ameongeza kuwa China inataka kuongeza ushirikiano na Misri katika chanjo ya COVID-19, na kuhimiza jumuiya ya kimataifa kushikamana kukabiliana na janga la COVID-19. Pia ameahidi kuunga mkono kampuni nyingi zaidi za China kuwekeza nchini Misri, na kupanua ushirikiano katika sekta za miundombinu, uzalishaji na teknolojia.

Naye rais al-Sisi amesema Misri na China ni marafiki wakubwa wa jadi, na zimedumisha ushirikiano wa karibu katika mambo ya kimataifa, Misri inaunga mkono China katika masuala ya Hong Kong, Xinjiang na Taiwan, na kupinga kithabiti vitendo vya kuingilia mambo ya ndani ya China kwa kisingizio cha haki za binadamu. Pia ameishukuru China kwa kuzisaidia nchi za Afrika na zile zinazoendelea kukabiliana na janga la COVID-19, na kutumai kuongeza ushirikiano na China katika suala la chanjo dhidi ya janga hilo.