Mamlaka nchini DRC zawatambua waasi wa FDLR waliohusika na kifo cha balozi wa Italia nchini humo
2021-02-23 16:34:16| cri

Mamlaka nchini DRC zawatambua waasi wa FDLR waliohusika na kifo cha balozi wa Italia nchini humo_fororder_VCG111318383545

Mamlaka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zimewatambua waasi wa kundi la FDLR la Rwanda waliohusika na shambulizi lililosababisha kifo cha balozi wa Italia nchini humo, Luca Attanasio.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo imesema, inadaiwa kuwa waasi hao walifanya shambulizi mapema jana, na kusababisha vifo vya watu watatu, akiwemo balozi Attanasio, mlinzi wake, na dereva wake raia wa DRC, huku wengine kadhaa wakijeruhiwa.

Gavana wa mkoa wa Kivu Kaskazini, Carly Nzanzu amesema, kutokana na ushuhuda uliotolewa na watu waliopona kwenye shambulizi hilo, waasi hao walidai fedha kutoka kwa balozi huyo.

Wakati huohuo, rais Felix Tshisekedi wa DRC amelaani vikali shambulizi hilo, na kulielezea kuwa ni la kigaidi lililochukua maisha ya balozi wa nchi rafiki wa DRC.