TENNIS: Djokovic atwaa taji la tisa na kuendeleza ubabe kwenye mchezo wa tennis
2021-02-23 15:36:49| cri

Mcheza tennis Novak Djokovic ameendeleza umahiri wake kwenye mchezo huo kwa kumbwaga Daniil Medvedev kwenye mechi ya Australian Open na kunyakua taji lake la tisa. Djokovic, 33, alimshinda Medvedev kwa seti 7-5, 6-2, 6-2 na kutwaa ufalme wa 18 wa Grand Slam, na kubakiza mataji mawili tu kuwafikia miamba wa dunia Roger Federer na Rafael Nadal. Nyota huyo raia wa Serbia anayenolewa na kocha Goran Ivanisevic, hajawahi kupoteza mechi yoyote ya Australia Open ugani Melbourne Park na ushindi wake dhidi ya Medvedev ulikuwa wa tatu mfululizo.