China yagundua akiba kubwa ya mafuta na gesi kwenye bahari ya Bohai
2021-02-23 08:46:48| CRI

China imegundua akiba kubwa ya tani milioni 100 za mafuta na gesi katika kisima cha 13-2 kilichoko katikati ya bahari ya Bohai, ugunduzi ambao una maana kubwa katika kuimarisha na kuongeza uzalishaji wa mafuta na gesi baharini na kuhakikisha usalama wa nishati nchini China.