Mtaalam wa WHO avilaumu vyombo vya habari vya Magharibi kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu ziara ya Wuhan
2021-02-23 18:21:26| cri

Mtaalam wa WHO avilaumu vyombo vya habari vya Magharibi kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu ziara ya Wuhan_fororder_VCG31N1230887138

Profesa Thea Kolsen Fischer wa kitengo cha magonjwa ya mlipuko ya kuambukiza katika Chuo Kikuu cha Copenhagen amevilaumu vyombo vya habari vya Magharibi kwa kutoa taarifa zisizo za kweli kuhusu ushirikiano wao na mamlaka nchini China.

Akihojiwa na gazeti la Politiken la Denmark, Profesa Fischer, ambaye alikuwa miongoni mwa timu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) iliyofanya ziara ya kutafuta chanzo cha virusi vya Corona mjini Wuhan, China, amesema takwimu nyingi zilikuwa zimeshaandaliwa wakati walipofika. Amesema timu hiyo na wenzao wa China waliheshimu maoni na uwezo wa kila upande, na kusifu ushirikiano kati ya timu ya WHO na wataalam wa China kuhusu takwimu na nadharia wakati wa utafiti wao uliodumu kwa mwezi mmoja.

Profesa Fischer amesema hayo kufuatia ripoti iliyochapishwa na gazeti la New York Times la Marekani Februari 12, inayowalaumu wanasayansi wa China kwa kukataa kutoa takwimu muhimu kuhusu mwanzo wa janga la virusi vya Corona, huku likiwanukuu watafiti huru wa WHO.