Gharama za usajili wa viwanda vipya, kikwazo kwa wajasiriamali
2021-02-23 15:33:15| cri

WAJASIRIAMALI wenye viwanda mkoani hapa, wamelalamikia gharama kubwa za usajili wanazotozwa na taasisi za serikali pindi wanapotaka kuanzisha viwanda vipya hali ambayo imekuwa ni kikwazo kikubwa kwao.

Wameeleza kuwa gharama hizo ni zile wanazotakiwa kulipa pindi wafuatiliapo vibali vya kuanzisha viwanda,leseni pamoja na ukiritimba wanaohupata katika shirika la viwangi nchini (TBS) pamoja na mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA) wanapohotaji kusajili bidhaa zao.

Waliyasema hayo juzi walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari katika mafunzo ya Kaizen,yana yoendelea katika ofisi za shirika la kuhudumia viwanda vidogo nchini (SIDO), Mkoani hapa.

Mafunzo hayo yaliwakutanisha wamiliki na wasimamizi wa viwanda vidogo 70, kutoka mkoani Arusha, yalifadhiliwa na Mfuko wa kuendeleza ujuzi (SDF) ulioko chini ya mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) na kuendeshwa na SIDO.

Mmiliki wa kiwanda cha kuchakata vyakula vya mifugo cha Mushono Farms,Hulda Kombe alisema kuwa hali hiyo imekuwa ikiwakatisha tamaa na kuwapa wakati mgumu katika kuendana na juhudi za serikali za Tanzania

ya Viwanda.

Kombe aliongeza kuwa changamoto nyingine ambazo wamekiwa wakikumbana nazo katika juhudi zao za kuanzisha viwanda ni riba kubwa wanazitizwa na taasisi za kifedha pondi waombapo mokopo kwa ajili ya kukuza mitaji yao na kuiomba serikali kuwapatia mikopo isiyo na riba.

Alilipongeza shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) mkoani hapa kwa mafunzo hayo na kueleza kuwa wamejifunza kuzalisha bidhaa bora zenye tija na viwango kwa mida mfupi na kwa gharama nafuu ikilinganishwa na hapo awali.