SOKA: Fenerbahce kumuweka sokoni Samatta
2021-02-23 15:37:29| cri

Nahodha na Mashambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Mbwana Ally Samatta huenda akaondoka Fenerbahce ya Uturuki, kufuatia kiwango chake kutoridhisha. Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika kutoka nchini Uturuki, Fenerbahce wameanza mipango ya kutaka kumpiga bei mshambuliaji huyo na kutafuta aliyebora zaidi, lakini wanasubiri na kujiridhisha kama ataweza kubadilika katika kipindi klichosalia kabla ya msimu huu haujafikia kikomo mwezi Mei.