Katibu mkuu wa UM ataka usawa katika ugavi wa chanjo ya COVID-19
2021-02-23 09:26:36| cri

 

 

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesisitiza kuwa ni lazima chanjo ya COVID-19 iwe bidhaa ya umma duniani, na ipatikane kwa usawa, kwa unafuu na kwa watu wote.

Kwenye mkutano wa 46 wa Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa, Bw. Guterres amesema usawa katika utoaji wa chanjo unathibitisha haki za kibinadamu, na utaifa wa chanjo ni kinyume na haki za kibinadamu.

Bw. Guterres amekutaja kushindwa hivi karibuni katika kuhakikisha usawa wa juhudi za chanjo kama "hasira ya kimaadili," kwani nchi kumi tu zimedhibiti zaidi ya asilimia 75 ya chanjo zote za COVID-19.