Tz: Biashara ya madini ifanyike kwenye masoko siyo hotelini- Samia
2021-02-23 15:32:33| cri

 

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, hapo jana amefungua Kongamano la kimataifa la Uwekezaji katika Sekta ya Madini lenye lengo la kutangaza fursa za Uwekezaji katika Sekta za Madini ziliopo Nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la uwekezaji katika sekta ya madini Samia amesema lengo ni kutangaza fursa na kuwaunganisha pamoja Wachimbaji na watoa huduma kwenye Shughuli mbalimbali zinazofanyika Migodini. Kongamano hilo la siku tatu lenye kauli mbiu “Sekta ya Madini kwa Uchumi Imara na Maendeleo Endelevu” limefunguliwa katika Kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere JNICC Jijini Dar es Salaam.

Amesema Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania ni wa muhimu kwani unaikutanisha Serikali na wadau wa sekta hiyo pia, ni jukwaa la kuujulisha ulimwengu kuhusu fursa za uwekezaji tulizonazo katika sekta hii.