Watu wenye silaha wawaua maofisa watatu wa polisi na kuwateka nyara raia kusini mashariki mwa Nigeria
2021-02-23 08:47:13| CRI

Maofisa watatu wa polisi wameuawa baada ya watu wenye silaha kushambulia bustani moja ya wanyama iliyoko kusini mashariki mwa Nigeria juzi Jumapili. Raia mmoja, ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa Bustani ya Wanyama ya Ogba jimboni Edo, alitekwa nyara kwenye shambulizi hilo. Mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa, na uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.