WHO na washirika wazindua mpango wa kutoa fidia kwa waathirika wa madhara ya chanjo katika nchi maskini
2021-02-23 08:46:20| CRI

Shirika la Afya Duniani WHO na washirika wake wamekubali kuzindua mpango wa kutoa fidia kwa watu waliopata madhara makubwa yanayotokana na chanjo ya COVID-19 katika nchi 92 zilizo nyuma kiuchumi. Taarifa iliyotolewa jana Jumatatu na WHO inasema, huu ni mpango wa kwanza na pekee wa kutoa fidia kwa waathirika wa chanjo katika ngazi ya kimataifa.