Idadi ya vifo vinavyotokana na COVID-19 nchini Marekani yapita laki tano
2021-02-23 08:45:49| CRI

Takwimu zilizotolewa na Chuo kikuu cha Johns Hopkins cha Marekani zinaonesha kuwa, hadi kufikia jana Jumatatu idadi ya vifo vinavyotokana na virusi vya Corona nchini humo imepita laki tano, huku idadi ya jumla ya maambukizi ikifikia milioni 28.1. Marekani inaendelea kuwa nchi iliyoathirika zaidi na janga la virusi vya Corona kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya maambukizi na vifo, ambayo inachukua asilimia 25 na asilimia 20 mtawalia ya ile ya dunia nzima.