Wang Yi ahudhuria mkutano wa ngazi ya juu wa kikao cha 46 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa
2021-02-23 17:11:14| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana amehudhuria mkutano wa ngazi ya juu wa kikao cha 46 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa.

Katika hotuba yake, Bw.Wang Yi amependekeza hatua za China katika kukabiliana na mabadiliko makubwa na janga kubwa la virusi vya Corona na kuhimiza na kulinda haki za binadamu. Ameelezea hatua hizo kuwa ni pamoja na kushikilia wazo la kuzingatia watu, kushikilia kuunganisha hali ya kawaida ya haki za binadamu na hali halisi ya nchi mbalimbali, kushikilia kuhimiza aina mbalimbali za haki za binadamu, na mwisho, kushikilia kufanya mazungumzo na ushirikiano wa kimataifa kuhusu haki za binadamu.

Bw. Wang Yi amesema, serikali ya China siku zote inatoa kipaumbele kwa usalama na afya ya kila mtu, na kulinda maisha na heshima ya watu. Amesema chanjo inahusiana na haki za afya, haki za maisha na haki za maendeleo ya watu, na inapaswa kusambazwa kwa usawa kote duniani, hasa kuhakikisha nchi zinazoendelea zinaweza kumudu gharama za chanjo hizo.