Mkutano kuhusu “Hadithi za Chama cha Kikomunisti cha China” wafanyika mkoani Xinjiang
2021-02-23 17:06:12| cri

Mkutano kuhusu “Hadithi za Chama cha Kikomunisti cha China” wafanyika mkoani Xinjiang_fororder___172.100.100.3_temp_9500032_1_9500032_1_1_7b42d949-837e-40ad-91f1-9e011b41efa5

Mkutano wa “Hadithi za Chama cha Kikomunisti cha China” umefanyika mjini Urumchi, mkoani Xinjiang, na kuhudhuriwa na viongozi na watu mashuhuri zaidi ya 310 kutoka vyama au mashirika zaidi ya 190 ya nchi zaidi ya 80 kwa njia ya video.

Pande mbalimbali zimefanya majadiliano ya kina na kufikia makubaliano kuhusu mada ya “ kwa ajili ya maisha mazuri ya wananchi”.

Tangu Mkutano mkuu wa Kamati Kuu ya 18 ya Chama cha Kikomunisti cha China ufanyike, maendeleo ya kiuchumi na kijamii yamedhihirika, na maisha ya wananchi mkoani Xinjiang yameboreshwa kwa kiasi kikubwa.

Katika mkutano huo katibu wa chama wa Mkoa Unaojiendesha wa Xinjiang Uygur Chen Quanguo alijulisha hadithi kuhusu maendeleo yenye kiwango cha juu ya uchumi, kuboreshwa kwa kiwango cha maisha ya wananchi, masikilizano kati ya dini mbalimbali, na kupambana na ugaidi na siasa kali mkoani humo.

Amesema yote yaliyofanyika mkoani Xinjiang ni kwa ajili ya kuwanufaisha wananchi wa makabila mbalimbali.