Chanjo ya Ebola kutoka WHO yawasili nchini Guinea
2021-02-23 16:08:55| cri

Wizara ya afya ya Guinea imesema, dozi elfu 11.5 za chanjo ya Ebola zilizotolewa na Shirka la Afya Duniani (WHO) zimewasili katika mji mkuu wa nchi hiyo, Conakry.

Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo imesema, chanjo hizo zitatumika kwa wakazi wa jimbo la N’zerekore, kusini mashariki mwa nchi hiyo.

Wakati huohuo, Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) kimetangaza kesi 14 za maambukizi ya Ebola nchini Guinea na Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC, ambapo watu 9 wamefariki kutokana na virusi hivyo.