Makubaliano ya nchi zenye mapato makubwa kuhusu chanjo yahatarisha mpango wa COVAX
2021-02-23 09:00:26| CRI

Mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Dk. Tedros Ghebreyesus, amesema baadhi ya makubaliano kati ya nchi zenye mapato mkubwa na mashirika yanayotengeneza chanjo ya COVID-19, yanahatarisha mpango wa utoaji chanjo duniani unaoongozwa na shirika hilo COVAX, kwani yanapunguza idadi ya chanjo ambayo mpango wa COVAX unaweza kununua.

Bw. Tedros amesema hata kama kuna fedha, mpango wa COVAX utaweza kutoa chanjo kwa nchi maskini kama nchi zenye mapato makubwa zitashirikiana kuheshimu makubaliano ya COVAX, na makubaliano mapya zinazosaini.

Amezitaka nchi zote, ikiwa ni pamoja na nchi zenye mapato makubwa, kuchangia chanjo haraka, na kuwataka watengenezaji wa chanjo kutoa kipaumbele kwenye mpango wa COVAX na kuongeza uzalishaji wa chanjo.