China yakaribisha nchi za Ulaya na Marekani kutoa chanjo kwa nchi za Afrika
2021-02-23 09:26:00| cri

 

 

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin, amesema China inakaribisha nchi za Ulaya na Marekani kutoa chanjo ya COVID-19 kwa nchi za Afrika, na kuzisaidia kushinda janga hilo.

Bw. Wang amesema China kutoa chanjo ya COVID-19 kwa nchi za Afrika kunaonesha urafiki wa jadi kati ya pande hizo mbili, pia ni hatua halisi ya utekelezaji wa ahadi ya rais Xi Jinping kuhusu kuifanya chanjo kuwa bidhaa ya umma duniani.

Bw. Wang ameongeza kuwa China imetoa chanjo ya COVID-19 kwa Guinea ya Ikweta na Zimbabwe, katika hatua ijayo itatoa msaada wa chanjo kwa nchi 19 za Afrika zenye mahitaji, na kwa nchi nyingi zaidi barani Afrika katika siku zijazo.