Watu 50 wafariki kwenye ghasia za gerezani Ecuador
2021-02-24 08:51:05| CR

Watu wasiopungua 50 walifariki jana Jumanne kwenye ghasia za gerezani zilizotokea katika mikoa mitatu nchini Ecuador.

Polisi nchini humo wamesema ghasia hizo zilizuka Jumanne asubuhi kutokana na mapambano kati ya magenge hasimu ya gerezani na mpaka sasa zimesababisha vifo vya wafungwa zaidi ya 50.

Waziri wa Serikali Patricio Pazmino amefanya mikutano na kamandi kuu ya polisi ili kuratibu hatua za kuhakikisha udhibiti wa magereza yote na kuzuia machafuko gerezani.