China yalaani shambulizi dhidi ya balozi wa Italia nchini DRC
2021-02-24 08:50:01| CRI

China imelaani vikali shambulizi lililosababisha kifo cha balozi wa Italia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Luca Attanasio akiwa kwenye ziara ya kibinadamu katika msafara wa Umoja wa Mataifa mkoani Kivu Kaskazini juzi Jumatatu.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema China inalaani vikali shambulizi dhidi ya wanadiplomasia na kutoa salamu za rambirambi kwa upande wa Italia kutokana na kifo cha balozi wao. Msemaji huyo ameitaka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuchukua hatua madhubuti mara moja kuboresha hali ya usalama kwenye sehemu yake ya mashariki na kulinda usalama wa raia wa China, wakiwemo wanadiplomasia wa China nchini humo.