“China kuweka mtego wa madeni barani Afrika”ni uwongo
2021-02-24 09:06:37| CRI

 

 

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin amesema “China kuweka mtego wa madeni barani Afrika” ni uwongo, China haikulazimisha nchi za Afrika kulipa madeni zinapokumbwa na changamoto za kiuchumi, na siku zote inapenda kutafuta utatuzi mwafaka kwa njia ya mazungumzo.

Kituo cha Utafiti wa Uhusiano kati ya China na Afrika cha Chuo Kikuu cha Johns Hopkins cha Marekani kimesema, baada ya kuchunguza nyaraka za makubaliano ya madeni kati ya pande hizo mbili, hawakupata ushahidi unaoweza kuthibitisha kuwa China itachukua mali za nchi za Afrika kama zikishindwa kulipa madeni.

Bw. Wang amesema China inatilia maanani kupunguza madeni au kuahirisha ulipaji wa madeni kwa nchi za Afrika, na hadi sasa imesaini au kufikia makubaliano na nchi 16 za Afrika kuhusu kuahirisha ulipaji madeni, na mbali na hayo, kutokana na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), China imezifutia madeni nchi 15 za Afrika ambayo yangelipwa mwishoni mwa mwaka jana.

Bw. Wang amesema suala la madeni ya nchi zinazoendelea lina historia ndefu na sababu tatanishi, na njia ya kimsingi ya kutatua suala hilo ni kuzisaidia nchi hizo kuongeza uwezo wa kujiendeleza.