Chombo cha anga za juu cha Tianwen-1 cha China chaingia kwenye mzunguko wa maegesho wa Mars
2021-02-24 18:22:37| cri

Chombo cha anga za juu cha Tianwen-1 cha China chaingia kwenye mzunguko wa maegesho wa Mars_fororder_eaf81a4c510fd9f92a12dbd95854cd222934a4ff

Mamlaka ya Anga za Juu ya China (CNSA) imesema, chombo cha anga za juu cha China, Tianwen-1 kimeingia kwenye mzunguko wa maegesho wa sayari ya Mars mapema leo.

Mamlaka hiyo imesema, chombo hicho kiliingia kwenye mzunguko huo majira ya saa 12.29 asubuhi kwa saa za China, na itachukua siku mbili za sayari ya Mars kukamilisha mzunguko kamili.

Mamlaka hiyo imeongeza kuwa, vifaa vyote vilivyopo ndani ya chombo hicho vitabadilishwa kwa ajili ya utafiti wa kisayansi.