Baadhi ya kampuni mjini Hangzhou zafuga wanyama vipenzi ofisini
2021-02-24 17:13:55| cri

Baadhi ya kampuni za mjini Hangzhou zimeanza kukumbatia utamaduni maalumu wa kimataifa wa kufuga wanyama vipenzi yaani “pets” wakiwemo mbwa na panya katika ofisi zao, kwa lengo la kuwapunguzia shinikizo na kuwaondolea uchovu wakiwa kazini.

Huu ni utamaduni wa kimataifa wa kuwafariji wafanyakazi unaofuatwa na kampuni nyingi kubwa za kimataifa kama vile Google, Amazon na Blizzard, ambazo wafanyakazi wao wanaruhusiwa kuwaleta mbwa wao ofisini.

Lakini kampuni hizo pia zimeweka kanuni kuhusiana na wanyama hao, kwa mfano ni lazima wanyama hao wapewe chanjo, lazimza wawe watulivu, hawaruhusiwi kwenda kwenye bwalo na mgahawa, hata wanatakiwa kuweka alama ya miguu yao kwenye mkataba wa kuhifadhi siri, ili kuhakikisha hawavujishi siri za kampuni…….