Guterres ataja maeneo manne ya kipaumbele ili kukabiliana na changamoto za tabia nchi zinazohatarisha amani na usalama
2021-02-24 08:46:31| CRI

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametaja maeneo manne ya kipaumbele kwa jumuiya ya kimataifa, ili kukabiliana na changamoto za tabia nchi zinazohatarisha amani ya usalama, kwanza ikiwa ni pamoja na kuweka mkazo kwenye hatua za kimazingira zenye nguvu na kabambe.

Hatua ya pili ameitaja kuwa ni kuchukua hatua za haraka za kuzilinda nchi, jamii na watu dhidi ya madhara yanayoendelea kuongezeka ya mabadiliko ya tabia nchi, yaani kuongeza uwezo wa kuendana na kuzoea mabadiliko hayo, na kuongeza uwekezaji.

Hatua ya tatu ameitaja kuwa ni kufuata wazo la usalama linalotoa kipaumbele kwa watu.

Bw. Guterres amesema COVID-19 imeonyesha jinsi yanayoitwa matishio yasiyo ya jadi yanavyoweza kuathiri dunia, na kutaka kuwe na ushirikiano zaidi ya mfumo wa Umoja wa Mataifa.