Thamani ya mali za kampuni zinazomilikiwa na serikali ya China katika nchi za nje yafikia yuan trilioni 8
2021-02-24 09:16:08| cri

 

 

Kamati ya usimamizi wa mali za taifa ya baraza la serikali la China, imesema hivi sasa thamani ya mali ya kampuni zinazomilikiwa na serikali ya China katika nchi za nje imefikia yuan trilioni 8, idadi ya taasisi na miradi ya kampuni hizo katika nchi na sehemu zaidi ya 180 imezidi 8,000, huku idadi ya wafanyakazi wao katika nchi za nje ikifikia milioni 1.25.

Mkurugenzi wa kamati hiyo Bw. Hao Peng amesema kampuni zinazomilikiwa na serikali kuu zimefanya juhudi na kushiriki kwenye ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, uwezo wao wa uendeshaji wa kimataifa umeongezeka, na zimehimiza maendeleo ya nchi iliko miradi yao.