Rais Xi atangaza "Ushindi Kamili” katika vita vya kutokomeza umasikini uliokithiri nchini China
2021-02-25 12:14:17| cri

Rais wa China Xi Jinping leo ametangaza kwamba China imepata "ushindi kamili" kwenye vita vyake vya kutokomeza umasikini.

Rais Xi ameyasema hayo leo wakati akihutubia mjini Beijing kwenye maadhimisho ya mafanikio ya nchi katika kuondoa umasikini na kuwaenzi wapiganaji wake wa mfano kwa kuondoa umasikini.

Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya jeshi, amesema umasikini uliokithiri umetokomezwa katika nchi hii yenye idadi kubwa ya watu duniani.

Katika miaka minane iliyopita, watu wa mwisho milioni 98.99 ambao ni wakazi masikini wa vijijini wanaoishi chini ya mstari wa sasa wa umaskini wote wameondolewa kwenye umasikini. Kaunti masikini 832 na vijiji maskini 128,000 vyote vimeondolewa kwenye orodha ya umaskini.

Kulingana na mstari wa sasa wa umasikini wa China, tangu China ianze mageuzi na kufungua mlango mwishoni mwa miaka ya 1970, wakazi milioni 770 wa vijijini ambao ni masikini wameondolewa kwenye umasikini.

China imechangia zaidi ya silimia 70 ya uondoaji umasikini duniani katika kipindi kama hicho. Rais Xi amesema, kwa mafanikio hayo, China imeleta “miujiza” mingine ambayo “itaandikwa kwenye vitabu vya historia”.

Rais Xi atangaza”Ushindi Kamili” katika vita vya kutokomeza umasikini uliokithiri nchini China

 

图片默认标题_fororder_图像_2021-02-25_121346