Takwimu zilizotolewa na Idara Kuu ya Takwimu ya China zinakadiria kuwa, mwaka jana wastani wa pato la taifa kwa mtu nchini China ulifika yuan elfu 72,447, sawa na dola za kimarekani karibu elfu 11.2, ambalo ni ongezeko la asilimia 2 ikilinganishwa na mwaka 2019.
Naibu mkuu wa Idara Kuu ya Takwimu ya China Bw. Sheng Laiyun amesema, mwaka 2020 Pato la Ndani (GDP) la China lilizidi yuan trilioni 100, sawa na dola za kimarekani karibu trilioni 15.45, na pato la taifa kwa mtu mmoja mmoja lilizidi dola elfu kumi za kimarekani kwa miaka miwili mfululizo, na uchumi wa China ulichukua zaidi ya asilimia 17 ya uchumi wa dunia katika mwaka 2020.
Takwimu hizo pia zinaonesha kuwa, mwaka jana China iliandikisha kampuni mpya zaidi ya milioni 25, na hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huo, idadi ya kampuni nchini China ilifikia milioni 140.