NDONDI: Kenya yasubiria nafasi zaidi Olimpiki
2021-03-01 16:01:57| cri

Licha ya Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) kufuta Mashindano ya Dunia kufuzu kushiriki Michezo ya Olimpiki, bara la Afrika lingali na afueni. Mashindano hayo yalipangwa kufanyika mwezi Machi jijini Paris nchini Ufaransa lakini yamefutwa kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo. Kulingana na naibu mkufunzi wa timu ya taifa ya ndondi nchini Kenya David Munuhe, bara la Afrika limepewa nafasi 11 ya mabondia watakaochaguliwa kushiriki michezo hayo. Amesema IOC itawachagua mabondia watakaoshiriki Michezo ya Olimpiki kulingana na viwango vyao, na kuongeza kuwa, huenda Kenya ikajiongezea nafasi mbili ama tatu katika idadi ya mabondia wawili ambao tayari wamefuzu kushiriki michezo hayo.