Mwanaume mmoja alikufa ghafla ndani ya saa 2 baada ya kuajiriwa, na familia yake ilidai fidia ya yuan milioni 1.4
2021-03-02 19:05:43| cri

Mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka jana, kutokana na oda nyingi, na ukosefu wa muda wa kutosha, Kampuni moja ya vifaa vya kinga mjini Shanghai ilimwajiri kwa haraka mwanamume mmoja aitwaye Li Mouwei kupitia kampuni moja. Saa nne na dakika 20 usiku wa Tarehe 29 Oktoba, Li aliingia rasmi kazini katika kampuni hiyo. Wakati alipofanya kazi hadi saa sita na dakika 25 alfajiri ya tarehe 30, alizimia ghafla na akapoteza fahamu.

Mfanyakazi mwenzake akapiga simu ya uokoaji na dakika 20 baadaye, gari la uokoaji lilifika kwenye eneo la tukio, wahudumu wa afya walijaribu kumwokoa Bw. Li lakini hatimaye alikufa. Wanafamilia walidai Bw. Li alifariki akiwa kazini, kampuni yake inatakiwa kuwajibika na kifo chake, na kudai fidia ya yuan milioni 1.4, sawa na dola za kimarekani laki 2.2. Msimamizi wa kampuni hiyo alieleza kusikitioshwa na tukio hilo, lakini anaona Bw. Li aliingia kazini saa mbili tu, na kampuni hiyo haikupanga kazi nzito kwake, na kwamba msiba huo ulisababishwa na hali ya afya ya mfanyakazi mwenyewe, kampuni haina kosa na inaweza tu kuwapatia wanafamilia wake mkono wa pole kwa sababu za kibinadamu. Msimamo wa kampuni uliwafanya wanafamilia wa Bw. Li wenye malalamiko makubwa wakasirike sana.