SMS yahimiza ulimaji kilimo cha viungo
2021-03-02 18:32:59| cri

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imewaataka wakulima kujikita kulima mazao ya viungo (spices) na matunda ambayo soko lake katika nchi nchi za nje lipo la uhakika. Hayo yamesemwa na katibu mkuu wizara ya Biashara na maendeleo ya viwanda, Dkt Islam Seif, wakati akizindua kamati ya ushauri ya utekelezaji wa mradi wa mazao ya viungo na kuwashirikisha wakurugenzi wa taasisi husika na sekta binafsi. Dk. Seif alisema ujio wa mradi wa viungo ni mkombozi kwa wakulima vijini ambao utasaidia  kupata kipato kikubwa na hivyo kumudu kuendesha familia na kupambana na umaskini. Aidha alisisitiza kuwa mradi huo utakuwa suluhisho la kutatua tatizo la ukosefu wa ajira katika kilimo cha viungo na utasaidia kukidhi ahadi ya rais ya kutoka ajira 300,000