SOKA: Kaizer Chiefs yafungwa 4-0 na Wydad Athletic
2021-03-02 16:35:15| cri

Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini imefungwa bao 4-0 na wenyeji Wydad Athletic ya Morocco kwenye mechi ya Klabu Bingwa Afrika iliyochezwa Jumapili. Katika mechi hiyo ya Kundi C iliyochezewa nchini Burkina Faso, Chiefs ilizamishwa na magoli yaliyofungwa na Mohamed Ounajem dakika ya saba, Ayoub El Kaabi (44), Mtanzania Simon Msuva (86) na Yahya Jabrane (90+2). Wydad kutoka Morocco imekalia juu ya jedwali kwa alama sita, Horoya ni ya pili kwa alama nne, Chiefs ina alama moja nayo Petro de Luanda haina kitu.