Wananchi wa Zimbabwe wasifu chanjo zilizotengenezwa na China
2021-03-02 16:40:33| cri

Wananchi wa Zimbabwe wasifu chanjo zilizotengenezwa na China_fororder_1127156563_16146498845471n

Jana, tarehe 1 Machi, rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ametoa hotuba kupitia televisheni, akisema msaada wa chanjo ya COVID-19 uliotolewa na China una umuhimu mkubwa katika kuwasaidia Wazimbabwe kujenga kingamwili mapema iwezekanavyo. Shehena ya kwanza ya msaada wa chanjo ya COVID-19 uliotolewa na China ulifika tarehe 15 mwezi uliopita katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare, na hivi sasa kazi ya utoaji wa chanjo nchini humo inaendelea kwa utaratibu, na wafanyakazi zaidi ya elfu 20 wamepewa chanjo hizo.

Hospitali ya Wilkins iko magharibi mwa Harare, mji mkuu wa Zimbabwe. Kabla ya saa tatu asubuhi, tayari watu wengi walikuwa wamepanga foleni kwenye eneo la kupewa chanjo. Baada ya kuthibitishwa na wahudumu wa afya na kuandikishwa, walipewa chanjo zilizotengenezwa na Kampuni ya Sinopharm ya China, na kupokea kitambulisho cha kupata chanjo.

Kwa mujibu wa mpango wa serikali ya Zimbabwe, utoaji wa chanjo utahusisha kwanza wahudumu wa afya, wafanyakazi katika sehemu zilizoko kwenye hatari kubwa zaidi ya kuambukizwa, na waandishi wa habari.

Gilbert Chiramba ambaye ni daktari, anaona kuwa utoaji wa chanjo ni njia yenye ufanisi katika kukabiliana na virusi vya Corona, akisema:

 “Kabla ya kupewa chanjo, nilisoma habari nyingi kuhusu virusi vya Corona, naona kuwa chanjo kutoka China zina usalama. Tumepewa chanjo nyingi tangu utotoni, nafahamu kuwa kupata chanjo ya virusi vya Corona ni njia yenye ufanisi ya kupambana na virusi, sina wasiwasi wowote.”

Willard Manungo ni mtumishi wa serikali. Alisema alikuwa na wasiwasi kidogo kabla ya kupewa chanjo. Lakini mchakato wa kupewa chanjo uliendelea kwa utaratibu, na anajisikia vizuri baada ya kupewa chanjo, na anapanga kuwahamasisha jamaa na marafiki wake kupewa chanjo.

Manungo anaishukuru serikali ya China kwa kuipatia Zimbabwe chanjo ya virusi vya Corona kwa wakati, na anaona kuwa chanjo hiyo itasaidia Zimbabwe kupambana na virusi. Akisema:

 “Naona kuwa chanjo za China zina usalama tena ufanisi. China ina kiwango cha juu cha utengenezaji wa dawa na mchakato wa kisasa wa maendeleo ya sayansi na teknolojia. Nina imani juu ya chanjo za China, pia natumaini kuwa wananchi wengine wataweza kupewa chanjo ili kushinda katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi.”