Marais wa China na Ufaransa wahudhuria na kuhutubia ufungaji wa mkutano wa kamati ya wajasiriamali wa China na Ufaransa
2024-05-07 09:09:42| CRI

Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron alasiri ya jana Mei 6 walihudhuria na kuhutubia ufunguaji wa mkutano wa sita wa kamati ya wajasiriamali wa China na Ufaransa.

Kwenye hotuba yake, Rais Xi amesema huu ni mwaka wa 60 tangu China na Ufaransa zianzishe uhusiano wa kibalozi. Katika miaka 60 iliyopita, nchi hizo mbili zimekuwa wenzi wa ushirikiano wa kunufaishana, na China imekuwa mshirika mkubwa wa kwanza wa kibiashara  kwa Ufaransa nje ya Umoja wa Ulaya.

Rais Xi amesisitiza kuwa, China ni mwakilishi muhimu wa ustaarabu wa Mashariki, huku Ufaransa ikiwa ni mwakilishi muhimu wa ustaarabu wa Magharibi. Katika hatua mpya ya maendeleo ya binadamu wakati dunia  inapokabiliwa na mabadiliko makubwa ambayo hayakutokea katika miaka 100 iliyopita, China inapenda kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na Ufaransa katika  sekta zote, na kusukuma mbele uhusiano kati ya nchi hizo mbili ufikie  kiwango cha juu zaidi na kupata mafanikio makubwa zaidi.