Waombaji wa kike wa fursa za ajira wadaiwa kuandika uzoefu wao wa mapenzi
2021-03-02 18:56:12| cri

Hivi karibuni kampuni moja iliwataka waombaji wa kike wa fursa za ajira kuandika uzoefu wao wa mapenzi, na muda wa kudumu kwenye uhusiano huo. Msimamizi wa kampuni hiyo alisema lengo la hatua hii ni kutathmini sifa ya kuweza kuajiriwa ya wafanyakazi, kwa kuwa takwimu za kampuni hiyo zimeonesha kuwa, wanawake wenye uzoefu wa kimapenzi na wale waliofunga ndoa wanafanya kazi kwa uhodari zaidi.

Wanamtandao wengi hawawezi kukubali dai hilo la kampuni. Lakini hii si mara ya kwanza kwa kampuni kutoa madai ajabu kwa watu wanaotafuta ajira. Kabla ya hapo, Kampuni moja ya biashara ya kielektroniki ilitoa dai la kutoajiri watu wanaoendesha gari la kampuni ya Volkswagen, na wale wanaoamini dawa za mitishamba. Kampuni moja ya mkoa wa Henan iliwataka waombaji wa fursa za ajira kuandika nyota zao na makundi ya damu zao katika C.V.